3. september 2010 Sitemap Print
 Søg
Reden International ni nani? 

Reden International ni shirika binafsi linalofanyakazi na wanawake wa nchi nyingine ndani ya Danmark. Tunafanyakazi mara nyingi na wanawake walioko kwenye umalaya na wanawake wanaonyanyaswa na kupigwa. 

Reden International wanafanya nini?

Reden International inafanya kazi katika ngazi ya mtaa na kuwapa wanawake msaada wa kidaktari, kisheria na mambo mengine ya kijamii. Tunaongea lugha 18, tunajua jinsi na wapi mtu anapata msaada kwa shida za ghafla, kwa mfano, ugonjwa, au kama mtu amenyanyaswa na kupigwa. 

RI inaendesha kituo kinachofunguliwa masaa 24 mbali na mazingira ya umalaya, ambapo mtu anaweza kupumzika na kupata nafuu baada ya matatizo na mapigo. 

RI inaendesha pia, pamoja na washiriki wetu wa kazi, mahali wanapokutania wanawake wa nchi nyingine, sehemu inakituo cha afya na hutoa misaada mengine ya kiafya. Hii iko katika mwendelezo wa ofisi yetu ilioko Colbjørnsensgade 12, Kopenhagen. 

Ni jinsi gani mtu anaweza kuwasiliana na Reden Internation?

Unamjua mwamke anayehitaji msaada, au unahitaji msaada mwenyewe, unaweza kupiga simu bila kujitambulisha katika namba zifuatazo: 

Reden International: +45 33 91 48 10 
Masaa 24 hotline inayopinga uuzaji wa watu: +45 70 20 25 50
Hotline ya polisi inayoshughulika na uuzaji wa watu: +45 45 15 06 08

Kama unataka kujua zaidi kuhusu sisi – au unahitaji msaada – unaweza pia kutembelea ofisi yetu: 

Reden International
Colbjørnsensgade 12, st.tv.,
1652 Kopenhagen V
Danmark 

Simu: +45 33 91 48 10
Fax: +45 33 91 04 73 

Email: info@redeninternational.dk
Website: redeninternational.dk